Home » Mgonjwa KNH Afariki Baada Ya Kuruka Kutoka Wadi Ya Ghorofa Ya 7

Polisi wanachunguza kisa ambapo mgonjwa alijitoa uhai kwa kuruka kutoka wadi ya ghorofa ya saba katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH)

 

Kwa mujibu wa walioshuhudia, tukio hilo lilitokea usiku wa kumkia leo hii Ijumaa wakati wagonjwa wengi walikuwa wamelala.

 

Mgonjwa huyo alikuwa amelazwa katika wadi nambari 7B kwenye ghorofa ya saba ya hospitali hiyo aliporuka hadi ghorofa ya chini na kufariki dunia papo hapo.

 

Maafisa wa usalama katika hospitali hiyo walisema walisikia kishindo kikubwa kwenye ghorofa ya chini na walipochunguza, walikuta mgonjwa tayari amefariki.

 

Walipigia simu polisi ambao walishughulikia eneo la tukio na kuuhamisha mwili kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.

 

Hospitali bado haijatoa taarifa kuhusu muda ambao mgonjwa alikuwa kwenye kituo hicho.

 

Aidha, sio mara ya kwanza kwa tukio kama hilo kutokea katika hospitali hiyo huku kukiwa na wito wa hatua zaidi kushughulikia hali hiyo.

 

Ghorofa ya saba na ya nane ya hospitali hiyo inahudumia wagonjwa wanaougua magonjwa ya kuambukiza kama vile malaria, UKIMWI, nimonia na Kifua Kikuu (TB).

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!