Home » UDA Kuanza Kusajili Wanachama Mtandaoni

Chama cha (UDA) kimefungua tovuti yake ya usajili mtandaoni huku kikianza harakati ya kukuza wanachama wake.

 

Chama cha Rais William Ruto chenye wanachama milioni 8.9 kimeapa kutumia kila mkakati ili kuhakikisha kuwa kinapata nguvu kuzingatia maandalizi ya uchaguzi wa 2027.

 

Chama hicho ambacho kiko katika mazungumzo na vyama vingine vya Kenya Kwanza ili kujipanga kabla ya uchaguzi ujao kimeongeza juhudi za kupenya ngome za kiongozi wa Upinzani Raila Odinga.

 

Kulingana na Katibu Mkuu mpya wa UDA Cleophas Malala, usajili huo utaanza Magharibi mwa Kenya wikendi hii kabla ya kuenea katika maeneo mengine ya nchi.

 

Shughuli hiyo inaendelea mjini Kisumu huku wanachama elfu 20,000 wakilengwa.

 

Malala ambaye amezungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa Kamati ya Utendaji ya Kitaifa katika Makao Makuu ya Chama,amesema hakuna juhudi zitakazoepukika kukuza UDA kuwa moja ya vyama vikubwa vya kisiasa nchini Kenya.

 

Mwenyekiti mpya wa chama Cecily Mbarire alisema ataangazia kuunda chama kitakachounganisha wanasiasa pamoja na kwakenya kwa ujumla

 

Malala alichukua nafasi ya Veronica Maina aliyeteuliwa katika seneti huku Mbarire akichukua wadhifa wa Seneta wa Machakos Johnson Muthama ambaye alijiuzulu wadhifa huo kufuatia kuteuliwa kwake katika Tume ya Huduma za Bunge (PSC).

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!