Rais Ruto Ashinda Tuzo ya Muungano Wa Viongozi Wa Kiafrika Dhidi Ya Malaria (ALMA).
Rais William Ruto Jumamosi, amepokea tuzo ya kimataifa alipokuwa akihudhuria Kikao cha Kawaida cha 36 cha Bunge la Wakuu wa Nchi na Serikali wa Muungano wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Mkuu wa Nchi alitunukiwa tuzo ya Muungano wa Viongozi wa Kiafrika wanaopigana dhidi ya ugonjwa wa Malaria (ALMA) tuzo la ”Joyce Kafanabo”.
Tuzo hiyo ilikuwa ya kutambua juhudi za Kenya katika kukuza huduma za afya miongoni mwa raia wake.
Ruto zaidi alitoa shukrani zake kwa rais wa Guinea Bissau Umaro Mokhtar Sissoco Embaló ambaye ni mwenyekiti wa ALMA.
Ruto aliahidi kuendelea kujitolea kutafuta mabadiliko chanya linapokuja suala la afya nchini.
Muungano wa Viongozi wa Kiafrika wa Malaria ni muungano wa kwanza wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika wanaofanya kazi katika nchi zote za Afrika.
Muungano huo unafanya kazi na mashirika na washirika mbalimbali kwa lengo la kutokomeza malaria barani ifikapo mwaka 2030.
ALMA mbali na Malaria pia inajitahidi kuondoa magonjwa muhimu ifikapo 2030.
Kupitia ajenda ya “Afrika Tunayoitaka”, ALMA inaweka kutokomeza malaria kama lengo kuu na Mfumo wa Kichocheo wa kukomesha virusi vya UKIMWI, Kifua Kikuu na Kutokomeza Malaria Barani Afrika ifikapo 2030.
Jana Rais William Ruto leo alitoa hotuba yake ya kwanza katika kikao cha 36 cha kawaida cha bunge la muungano wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia, ambapo alitoa shukrani zake kwa A.U kwa kusimama na Kenya.
Rais Ruto ambaye anahudhuria mkutano huo wa siku 3 alitoa uungaji mkono wake kwa eneo la Afrika kwa manufaa ya watu wake.