Home » Kenya Yarekodi Vifo 85 Vya Kipindupindu, Maafisa Wahimiza Tahadhari

Kenya Yarekodi Vifo 85 Vya Kipindupindu, Maafisa Wahimiza Tahadhari

Kenya imerekodi visa  4,821 vya kipindupindu na vifo 85 tangu kuzuka kwa ugonjwa huo Oktoba 10 mwaka jana, huku wasiwasi ukiibuka kuhusu kaunti kukosa vifaa vya kupima ugonjwa huo.

 

Ugonjwa huo ambao uliripotiwa mara ya kwanza Limuru, Kaunti ya Kiambu – Oktoba 8, unaendelea kuenea na sasa umerekodiwa katika kaunti 15.

 

Kulingana na ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya Februari 14, Kenya ni miongoni mwa nchi tano bora barani Afrika zenye idadi kubwa ya maambukizi kufikia sasa vifo vya visa hivyo nchini ni asilimia 1.8.

 

Wakati wa mkutano kuhusu mlipuko wa kipindupindu barani Afrika, Mtaalamu wa Magonjwa ya Kanda ya Afrika wa WHO – Patrick Otim alisema maambukizi yamesababishwa na hali mbaya ya hali ya hewa na kusababisha ukame au mafuriko.

 

Kulingana na Wizara ya Afya, Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa vifo 29, ikifuatiwa na Tana River na vifo 17.

 

Garissa imepoteza watu 12, Wajir (tisa), Kiambu (watano), Machakos na Kitui (wanne kila mmoja), Meru (watatu) na Homa Bay wawili.
Ugonjwa huo umeenea katika kaunti za Nairobi, Kiambu, Nakuru, Kajiado, Uasin Gishu, Muranga, Machakos, Garissa, Wajir, Meru, Nyeri, Tana River, Kitui, Homa Bay, Mandera na Pokot Magharibi.

 

Garissa inaongoza kwa visa elfu 2,012. Tana River imerekodi visa mia 730, ikifuatiwa na Nairobi mia (624), Kiambu mia (380), Wajir mia (326), Machakos mia (268) na Mandera mia (219).

 

Kaunti ya Nakuru imeripoti wimbi la tatu la ugonjwa wa kipindupindu huko Naivasha visa nne mpya vimeripotiwa Nakuru kufikia jana.
Aidha, hospitali jijini Nairobi zimeanza kuchukua tahadhari kuhakikisha ugonjwa huo unadhibitiwa huku Kaunti kadhaa zikisitisha uuzaji wa chakula. ..Shule, kwa upande mwingine, zinatoa chanjo ya mdomo kwa watoto.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!