Home » Mudavadi Alaani Kuongezeka Kwa Mimba Za Mapema Magharibi Mwa Nchi

Waziri mwenye mamlaka Musalia Mudavadi anasema takwimu zinazoonyesha kuongezeka kwa visa vya mimba za mapema nchini zinathibitisha kwamba wasichana wanasalia katika hatari ya kudhulumiwa.

 

Mudavadi ambaye amezungumza wakati wa kongamano la kwanza la wanawake Magharibi mwa Kenya lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro katika Kaunti ya Kakamega, ametaja data inayoonyesha kuwa mtoto wa kike leo yuko katika hatari kubwa ya kupata mimba, huku kukiwa na ufichuzi kuwa kaunti za Bungoma, Busia, Trans Nzoia, Vihiga na Kakamega zinasajili vingi kitaifa.

 

Takwimu za kuhuzunisha zinaonyesha kuwa ingawa hatari ya kitaifa kwa mtoto wa kike iko katika asilimia 14.9 kwa jumla, eneo la Magharibi mwa Kenya lina viwango vya kutisha huku Kaunti ya Bungoma ikirekodi asilimia 18.6, Busia asilimia 18.3, Trans Nzoia asilimia 17.8, Kakamega asilimia 15.1 na Kaunti ya Vihiga asilimia 7.7.

 

katika toleo la hivi majuzi la Utafiti wa Demografia na Afya ya Kenya, Kaunti ya Nairobi ambao ni Mji Mkuu wa Kenya pia umerekodi asilimia kubwa ya 8.4 ambayo bado ni kiwango cha kutisha.

 

Kuhusu uwezeshaji wa jumla wa wanawake wa Kenya, Mudavadi amebainisha kuwa kutakuwa na mabadiliko makubwa katika sera.
Huku akitoa changamoto kwa wanawake kuchukua uongozi katika kuwezesha mtoto wa kike, kuwalinda, na kuwaelekeza kwenye njia salama, Waziri Mkuu ametoa mfano wa msichana mdogo kutoka Lugari katika Kaunti ya Kakamega ambaye alilazimishwa kuwa mama baada ya kuolewa na mzee wa miaka 72.

 

Msichana huyo, aitwaye Cynthia, alisimulia jinsi alivyoachwa yatima katika umri mdogo na kulazimishwa kuwa mama akiwa na umri wa miaka 13 kutokana na kukosa usaidizi wa wazazi.

 

Mudavadi amesema pia kuna haja ya dharura ya kuanza kampeni kali dhidi ya Ukimwi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!