Home » Rais Ruto Ateua Jopokazi La Kitaifa La Bahati Nasibu

Rais William Ruto ameanzisha jopokazi la wanachama 27 litakaloongoza uanzishaji wa bahati nasibu ya kitaifa kulingana na Ajenda ya Kenya Kwanza ya Mabadiliko ya Kiuchumi (BETA).

 

Kwa mujibu wa notisi ya Gazeti la tarehe 17, mkuu huyo wa nchi alitangaza kuunda programu hiyo ya bahati nasibu ambayo alisema itaongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali ili kusaidia kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.

 

Wajumbe hao wamegawanywa katika makundi mawili, kamati ya uongozi iliyojumuisha wajumbe 14 na kamati ya ufundi iliyojumuisha watu 10 watakaohudumu katika kikosi hicho kwa muda wa miezi mitatu.

 

Kundi la kwanza la wajumbe sita wa kamati ya uongozi linajumuisha Makatibu Wakuu wanne au wawakilishi wao, Mwanasheria Mkuu au mwakilishi wake na mwakilishi wa baraza la magavana.

 

Wakurugenzi hao wanatoka katika wizara nne zikiwemo Hazina, Mambo ya Ndani, Utamaduni ,, Urithi na Ulinzi wa Jamii.
Dkt Narendra Raval aliteuliwa kuwa mwenyekiti huku Gideon G. Thuranira akiwa naibu wake.

 

Wanachama wengine ni Paul Russo, Judith Karigu Kiragu, Anne Wakathiru Njenga, Grace Kamau, Abdillahi K. Mutwafy na Jackline Chelangat Tonui.

 

Wanachama 10 wa kamati ya kiufundi ambayo itaongozwa na Dkt Linda Musumba ni Wanjiku Wakogi, Dkt Eric Aigula, Collins Kiprono, Peter Mbugi, Fred Mbasi, Geoffrey Malombe, Eric Korir, Wilson Njenga, Catherine Ochanda na Murimi Murage.

 

Clinton Mwita na Margaret Githaiga walichaguliwa kuwa Makatibu Muhtasi katika kamati iliyotajwa hapo juu.

 

Miongoni mwa majukumu muhimu ya kikosi kazi ambacho usimamazi wake utakuwa na makao yake Ikulu ni kufanya mapitio ya kina ya mbinu bora za uanzishaji wa bahati nasibu za Taifa na kuandaa sera na mpango wa utekelezaji utakaoongoza uendeshaji wa Bahati nasibu ya Taifa katika Kenya.

 

Notisi hiyo pia inasisitiza kwamba wanachama watawezesha mashauriano na washikadau wote wakuu na kuchunguza miundo iliyopo ya kiutawala, kitaasisi, sera na sheria katika tasnia ya kamari na michezo ya kubahatisha na kupendekeza marekebisho ya kina.

 

Yakijiri hayo Kinara wa Azimio Raila Odinga ameendeleza kampeni za kupinga uongozi wa rais William Ruto na kufanya mkutano katika kaunti ya Kisumu ambapo aliwataka wenyeji kutokubali sera zozote za serikali ya Kenya Kwanza.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!