Home » Rais Ruto Akutana Na Magavana Naivasha

Rais William Ruto leo Ijumaa anatarajiwa kufanya mkutano na magavana wote wa kaunti huku kukiwa na mzozo wa kifedha kati ya wakuu wa kaunti na serikali.

 

Mkutano huo wa siku mbili huko Naivasha, Kaunti ya Nakuru uliopewa jina la Mkutano wa Tisa wa Kuratibu Serikali ya Kitaifa na Kaunti utamshuhudia mkuu wa nchi akishughulikia maswala yanayohusu mzozo wa kifedha nchini.

 

Naibu Rais Rigathi Gachagua, Baraza la Mawaziri na Makatibu Wakuu pia wanatarajiwa kupamba kongamano hilo.

 

Masuala mengine yanayotarajiwa kujadiliwa ni pamoja na masuala ya kikatiba, ugatuzi wa kazi na rasilimali, miswada muhimu inayohusu serikali za kaunti, ripoti za ukaguzi na kesi mahakamani kati ya ngazi hizo mbili za serikali.

 

Mkutano huo unajiri wiki moja tu baada ya naibu rais Gachagua kuwakashifu magavana kuhusu madai yao ya kutaka mgao wa kaunti uongezwe kutoka Ksh.370 bilioni hadi Ksh.425 bilioni.

 

Naibu Rais alisema utawala unaoongozwa na Rais Ruto haukuweza kutimiza matakwa yao na ungetenga tu kati ya Ksh. 380 na Ksh.385 bilioni.

 

Magavana hao ambao wamekuwa wakikashifu madeni katika kaunti na mrundikano wa malipo wamekuwa wakishinikiza nyongeza hiyo ili kuwaruhusu kufuta bili ambazo hazijakamilika na kurahisisha utoaji huduma kwa Wakenya.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!