Home » Waziri Ezekiel Machogu Azungumzia Video ya Adhabu ya Wanafunzi Kisii

Waziri Ezekiel Machogu Azungumzia Video ya Adhabu ya Wanafunzi Kisii

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amesema walimu sita kutoka Shule ya Msingi ya Itumbe D.O.K wanaoshutumiwa kutekeleza adhabu chafu kwa wanafunzi watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Akizungumza na vyombo vya habari asubuhi ya leo Machogu amethibitisha kuwa walimu hao pia wataachishwa kazi iwapo watapatikana na hatia ya uhalifu unaofanywa dhidi yao.

Katika video hiyo ambayo imesambaa kwa kasi mitandaoni , walimu waliwalazimisha wanafunzi kufanya vitendo vichafu huku wakiwa wamelala juu ya kila mmoja.

Walimu hao pia wanasikika wakitishia kuwachapa wanafunzi hao iwapo watashindwa kufanya vitendo hivyo.

Mkurugenzi wa Kaunti Ndogo ya Nyamache Linet Onduso baadaye alithibitisha kwa vyombo vya habari kwamba walimu hao sita walikamatwa wakisubiri uchunguzi wa kisa hicho.

Afisa mkuu wa polisi kaunti ndogo ya Nyamache Kipkemoi Kipkulei pia amethibitisha kuwa simu za walimu hao zilitwaliwa ili kuchunguza dhamira ya kurekodi video hiyo na kuiweka mtandaoni.

Kulingana na Kipkulei, mmoja wa walimu hao alifichua kuwa wanafunzi hao waliripotiwa kufanya vitendo hivyo wakati wa mapumziko na hivyo walikuwa wanachunguza kile ambacho wanafunzi hao walifanya.

Wakenya wameelezea ghadhabu zao kuhusu mienendo ya walimu hao huku wengi wao wakiitaka Wizara ya Elimu kuwachukulia hatua kali.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!