Home » Jeremiah Kioni Akashifu Uongozi Wa Rais William Ruto

Katibu Mkuu wa Chama cha Jubilee Jeremiah Kioni amemkashifu Rais William Ruto kwa kuongoza taifa bila kujua mwelekeo maalum.

Kulingana na Kioni, Rais Ruto amewahadaa Wakenya kwa vile ahadi zake za kampeni hazijazaa matunda yoyote ilhali taifa linahitaji maendeleo kwa sasa.

Kioni alifananisha uongozi wa Rais Ruto na gari lisilokuwa na mwelekeo na kwamba taifa litapata madhara makubwa iwapo atalielekeza katika njia mbaya.

Mwanasiasa huyo amesisitiza zaidi kwamba muungano wa Azimio la Umoja, ambao sasa uko katika upinzani, utakuwa thabiti kuikemea serikali kila inapokosea na kuidhibiti.

Wakati huo huo, Kioni amebainisha kuwa mikutano ya hivi majuzi ya Azimio ambayo kufikia sasa imeandaliwa katika viwanja viwili jijini Nairobi, haitakoma na itafanyika katika kila pembe ya taifa.

Hata hivyo, amedokeza kuwa miongoni mwa mikutano hiyo, mmoja umepangwa kufanyika Kibera jijini Nairobi na mwingine Machakos.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!