Mazungumzo Yafeli Kuhusu Mgao Wa Fedha Za Kaunti
Serikali kupitia Hazina ya Kitaifa imetenga Ksh. bilioni 380 kwa serikali za kaunti badala ya shilingi bilioni mia 425 zilizopendekezwa na Tume ya Ugavi wa Mapato (CRA).
Kiasi hicho kilipuuza si mapendekezo ya CRA pekee bali pia ahadi ya Rais William Ruto aliyoitoa katika kampeni ya Agosti 2022.
Rais Ruto alikuwa ameahidi kwamba iwapo atachaguliwa kuwa rais, ataongeza mgao wa mapato ya kaunti kutoka asilimia 15 iliyoidhinishwa na katiba hadi asilimia 35.
Ahadi hiyo iliwasilishwa Januari 24, 2022, wakati wa mkutano wa Kikundi cha Wabunge wa United Democratic Alliance (UDA) uliofanyika katika makazi yake ya wakati huo Karen.
Naibu mwenyekiti wa baraza la magavana ambaye pia ni Gavana wa Wajir Ahmed Abdullahi amelalamika kwamba ukomo wa bajeti ya wizara za serikali ya kitaifa haujasawazishwa ili kuhakikisha mipango muhimu ya kipaumbele ambayo imegawiwa kikamilifu inaendana sawa na mgao wa mapato katika serikali za kaunti.
Kifungu hicho kinaangazia vigezo ambavyo vitazingatiwa katika kubainisha hisa zinazolingana kati ya serikali ya kitaifa na kaunti.
Kulingana na kifungu hicho, usambazaji lazima uzingatie mahitaji ya maendeleo ya kaunti.