Home » Mbunge Atandi: Ruto, Gachagua Wakomeshe Kampeni Za Kisiasa

Mbunge Atandi: Ruto, Gachagua Wakomeshe Kampeni Za Kisiasa

Mbunge wa Alego Usonga katika kaunti ya Siaya Sam Atandi amewataka Rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua kukoma kujihusisha na siasa na kulenga kusimamia majukumu yao ya uongozi.

Akiongea kwenye kipindi cha Runinga moja humu nchini, Mbunge Atandi amebainisha kuwa wawili hao wanafaa kutambua kuwa wana vyombo vya mamlaka na sasa wanapaswa kuanza kushughulikia kuwasilisha huduma kwa Wakenya.

Mbunge huyo ameongeza kuwa taifa liko katika hali mbaya na kujihusisha na siasa kutakwamisha kutafuta suluhu ya mzozo wa kiuchumi.
Atandi amebainisha kuwa serikali inafaa kuangazia miale yake katika kutatua gharama ya juu ya maisha na kufanya mashauriano na Wakenya ili kudumisha umoja.

Vile vile, ameonya kuwa serikali inafaa kupunguza viwango vya ushuru ambavyo anasema vinaathiri mifuko ya Wakenya kutokana na hali ya uchumi ambayo haijaimarishwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!