Home » Rais Ruto Awasuta Wawakilishi Wadi Wa Kericho

Rais Ruto Awasuta Wawakilishi Wadi Wa Kericho

Rais na Naibu wake wafika Bomet Green Stadium kwa ajili ya ibada Jumapili January 15,2023.

Rais William Ruto amewasuta viongozi waliochaguliwa kwa kupigania nyadhifa za uongozi katika bunge la kaunti ya Kericho.

Akizungumza wakati wa Ibada ya kanisa katika uwanja wa Green Stadium katika Kaunti ya Bomet, Rais Ruto ametoa wito kwa wawakilishi wadi wa Kaunti ya Kericho kuacha  kuzozania nyadhifa za uongozi wa bunge hilo na badala yake kuwahudumia wapiga kura.

Ruto ambaye matamshi yake yamejiri siku chache baada ya video ya fujo katika Bunge la Kaunti ya Kericho kusambaa, amewataka viongozi hao kukoma kupoteza muda na kutanguliza kuwasilisha miswaada ya kutimiza ahadi zao za kampeni.

Amesema upinzani haujawekwa kwa ajili ya wapiga kura bali kwa nia ya kuwapiga msasa kila wakati viongozi waliochaguliwa Katiba na hivyo kuweka udhibiti wa serikali.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!