Home » Serikali Yahimizwa Kutumia Simu Kupokeza Wazee Pesa Za Inua Jamii

Serikali Yahimizwa Kutumia Simu Kupokeza Wazee Pesa Za Inua Jamii

Serikali imetakiwa kutafuta mbinu za kuwatumia wazee wakongwe pesa za Inua Jamii kwenye simu zao badala ya kutumia benki.

Haya yanajiri baada ya wakongwe watatu ikiwemo mwanamme mmoja na wanaume wawili kuuawa katika muda wa wiki moja baada ya kupokea pesa hizo.

Huko Baringo ya Kati, mkaazi mzee mwenye umri wa miaka 70 alipatikana ameuawa ndani ya nyumba yake na Ksh.8,000 alizopokea kuibiwa.

Cherutich Cherono aliyekuwa akiishi peke yake katika kijiji cha Kitumbei, alivaamiwa na watu wasiojulikana walipomvamia na kumuua mnamo Ijumaa, siku 5 tu baada ya kupokea pesa alizokusanya.

Kisa hicho kinajiri siku tatu baada ya mzee wa miaka 90 kuuawa kinyama na watu wasiojulikana na kumnyang’anya pesa zake huko Kibwezi, Kaunti ya Makueni huku nyanya mmoja akiteketezwa na mjukuu wake huko Trans zoia baada ya kukataa kumpa pesa alizopokea kwenye mpango wa Inua Jamii.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!