Home » Mpiga Debe Mandonga Anatamba

Mwanandondi Karim Mandonga /picha kwa hisani/

Maisha ya bondia machachari wa Tanzania Karim Mandonga yamebadilika ghafla kinyume na matarajio yake.

Kabla ajiunge na ndondi za kulipwa mwaka wa 2015, Mandonga alikua anafanya kazi ya kushawishi abiria waingie kwa mabasi ya Aboud mjini Morogoro anakotoka.

Nchini Tanzania wanao fanya kazi hiyo wanajulikana kama wapiga debe na makanga nchini Kenya.

Maneja wa Mandonga Juma Ndambire anasema bondia wake amepiga hatua kubwa kutokana na kipaji chake cha mauzo.

“Nchina Tanzania Mandonga ni brand sasa, ana mkataba na kampuni ya Wasafi Bet, Robi One na K4 Security,” anasema Ndambire akiongezea kwamba kuna makampuni kadhaa yanamtaka Mandonga kwa madhumuni ya mauzo ya bidhaa zao.

“Baada ya ushindi wa Mandonga dhidi ya Daniel Wanyonyi tumealikwa England, Msumbuji na Mauritius wote wanataka Mandonga apigane huko,”aliongezea Ndambire.

Kulingana na Ndambire, Mandonga, mwenye umri wa miaka 43, alianza ndondi mwaka wa 2000.

“Nia yake ya kujifunza ndondi ilikua ni ya kujikinga tu, na mabondia walomvutia sana ni Mike Tyson na Floyd Mayweather Jr. Kwa kweli Mandonga mwenyewe anapenda ndondi. Ziko kwa damu. Baada ya pigano lake na Said Mbelwa mwaka jana mchezo wake sasa umeimarika zaidi. Tutarudi Kenya mwezi wa nne huenda Mandonga akapambana na Rayton Okwiri,” alisema

Ndambire na bondia wake wanasafiri leo, January 16, kurudi nyumbani Tanzania

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!