Home » Prof. Kibwage Alaumu Ufadhili Wa Serikali Kwa Wanafunzi Wa Vyuo Vikuu

Prof. Kibwage Alaumu Ufadhili Wa Serikali Kwa Wanafunzi Wa Vyuo Vikuu

Naibu Chansela wa Chuo Kikuu cha Egerton Prof. Isaac Kibwage amesema kutokana na serikali kusaidia wanafunzi wote wanaoingia chuo kikuu, vyuo vikuu vya umma kote nchini vimekabiliwa na changamoto za kuendeleza shughuli zake kwani mapato yao hayawezi kuendana na gharama za programu.

Akizungumza na wanahabari, Profesa Kibwage amewasuta wahadhiri wanaonyoshea kidole cha lawama usimamizi wa chuo hicho kwa kutowalipa mishahara yao kwa aslimia 100 kama ilivyoagiza mahakama, akisema wanafanya hivyo pasi na kuchunguza kiini haswa cha tatizo la chuo hicho kukosa fedha.

Wakati  huo huo Prof. Kibwage amedokeza  kuwa uongozi wa chuo unatafakari kufuta baadhi ya programu ambazo hazijawavutia wanafunzi kwa miaka mitano iliyopita.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!