Home » Wakenya Wanaopitia Madhila Nchi Za Kigeni Hujihusisha Na Biashara Haramu

Wakenya Wanaopitia Madhila Nchi Za Kigeni Hujihusisha Na Biashara Haramu

Waziri wa Maswala ya Kigeni Dkt. Alfred Mutua amefichua kuwa kuna Wakenya wanaoishi ughaibuni ambao hujihusisha na biashara haramu ili kujipatia riziki katika baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati ambako hata unywaji na utengenezaji wa pombe ni kinyume cha sheria.

Akizungumza na wahandishi wa habari hapa nchini, Dkt. Mutua huku akiwapongeza Wakenya kwa ubunifu wao katika masuala ya biashara, aliangazia kidogo suala la jinsi baadhi ya watu wanavyojihusisha na vitendo vya uvunjaji sheria ambavyo vimesababisha baadhi ya mateso ya raia wanaoishi nje ya nchi, haswa katika Ghuba.

Mutua amesema wengi wa wakenya ambao husema wanateswa, huwa wametoroka kutoka kwa waajiri  wao, na hawawezi kwenda hospitalini kwa hofu ya kufurushwa na kurejeshwa nyumbani.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!