Home » EACC Yachunguza Madai Ya Ulaghai Wa Ununuzi Katika Chuo Kikuu Cha Pwani

EACC Yachunguza Madai Ya Ulaghai Wa Ununuzi Katika Chuo Kikuu Cha Pwani

Tume ya Maadili na Kupambana na ufisadi EACC imeanzisha uchunguzi kuhusu tuhuma za udanganyifu wa taratibu za ununuzi katika Chuo Kikuu cha Pwani.

 

Taasisi hiyo inakabiliwa na shutuma za kupendelea kampuni moja ya bima katika kutoa zabuni za bima ya matibabu ya wafanyikazi.
Katika barua iliyoonekana na Billy o’clock.co.ke na kutumwa kwa Naibu Chansela wa taasisi hiyo, Afisa Mkuu wa Upelelezi wa EACC, Tabu Lwanga amesema madai hayo yamedumu kwa miaka mingi sasa.

 

Lwanga amemtaka naibu chensela kuhakikisha kuwa zabuni zozote zinazohusiana na hizo zinazotolewa wakati uchunguzi ukiendelea zinafanyika kwa kufuata sheria.

 

Katika tuhuma hizo, Chuo Kikuu cha Pwani kinadaiwa kutumia manunuzi ya moja kwa moja kutoa zabuni hiyo kwa Kampuni ya Bima inayokiuka sheria.

 

Afisa huyo wa EACC ameonya kwamba ikiwa uchunguzi utathibitisha kwamba taasisi hiyo kweli ilikiuka sheria, huenda ikakabiliwa na mashtaka ya jinai.

 

Miongoni mwa majukumu ya EACC ni kufanya uchunguzi kuhusu ufisadi, uhalifu wa kiuchumi na utovu wa maadili.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!