Home » Kenya Kwanza Yatishia Azimio

Timu ya Kenya Kwanza ya mazungumzo ya pande mbili Bipartsan sasa inataka Jopo la Uchaguzi la tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kuendelea na kuajiri makamishna wapya hata kama upande wa Azimio utakosa kuhudhuria mkutano wiki ijayo.

 

Wakiongozwa na mwenyekiti mwenza wa Kamati ya Pamoja George Murugara, Kenya Kwanza wamesema wameimpa Azimio nafasi ya mwisho Jumanne wiki ijayo.

 

Murugara amesema iwapo upinzani utasusia mkutano wa wiki ijayo, sheria itachukua mkondo wake.

 

Wakihutubia kikao na wanahabari katika majengo ya Bunge, timu ya Kenya Kwanza ikiongozwa na Mbunge wa Tharaka imeshutumu mrengo wa Azimio kwa kupotosha umma nan chi kwa ujumla.

 

Kuajiri makamishna ilikuwa mojawapo ya ajenda za Kamati ya pamoja iliyoundwa kumaliza maandamano dhidi ya serikali yaliyofuatia uchaguzi wa urais wa Agosti 9.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!