Home » Wanasiasa Wa Azimio Watoa Wito Wa Maandamano

Washirika wa Azimio wamezidisha wito wa kuchukuliwa hatua kwa wingi juu ya gharama ya juu ya maisha nchini

 

Wakizungumza katika uwanja wa Kamkunji ambako Upinzani uliitisha mkutano wa ‘mashauriano’ na wananchi, wanasiasa hao wamesema maandamano ndiyo lugha pekee ambayo serikali inaelewa.

 

Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amesikitika kwamba utawala wa Kenya Kwanza haujaonyesha nia ya kushughulikia maswala ya wananchi.
Aidha kinara wa Azimio Raila Odinga amesema kwa sasa watashinikiza serikali hadi iwasikie wakenya na kuendelea kusuta utawala wa Kenya kwa kupandisha uchumi hadi zaidi.

 

Waliokuwepo ni wabunge Anthony Oluoch, Beatrice Ogolla, Beth Siengo, Otiende Amollo, Millie Odhiambo, Tim Wanyonyi, Babu Owino, Godfrey Osotsi, Enoch Wambua, na wawakilishi wengi wa wadi.

 

Wambua amesema juhudi za Azimio kuhakikisha kero za wananchi zinashughulikiwa kupitia Bunge hazijafanikiwa kutokana na idadi kubwa ya wabunge wa Kenya kwanza.

 

Kiongozi wa Wachache katika Seneti Stewart Madzayo kwa upande wake wanasiasa “wasinzi” wanapaswa kukabiliwa na uchaguzi mdogo katika maeneo bunge yao na kudai kuwa wabunge ambao ni rafiki kwa utawala wa rais William Ruto hawahitajiki Azimio.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!