Home » Azimio Yaamuru Wakenya Kutolipa Ushuru

Azimio la Umoja imetangaza msururu wa maazimio ya kukabiliana na Rais William Ruto, ambaye alipuuza matakwa yao kuhusu Sheria ya Fedha ya 2023.

 

Katika taarifa ambayo ilisomwa na Kiongozi wa Chama cha Democratic Action Party (DAP) Kenya Eugine Wamalwa, Azimio imetoa wito wa kutolipa ushuru kuanzia Julai 7, 2023.

 

Muungano huo umeeleza kuwa wataanza mchakato ambao utafikia kilele cha kuondolewa kwa serikali ya Kenya Kwanza kutoka kwa mamlaka.

 

Kwa sasa macho yote yanaelekezwa katika mazungumzo ya pande mbili huku sasa wakenya wakisubiri kuona iwapo Kenya kwanza watajibu madai ya azimio au la.

 

Ikumbukwe tayari rais William ruto amesema haishutuliwi na maandamano ya upinzani kivyovyote huku naibu rais rigathi gachagua akidai kwa sasa hamna nafasi ya kuhusisha upinzani katika utawala wa Kenya kwanza.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!