Home » Shakilla Amjibu Sherlyne Anyango

Sosholaiti wa Kenya Shakilla Tiffany amejibu baada ya sosholaiti mwenzake na mwanamuziki Sherlyne Anyango kueleza jinsi maisha yamekuwa tangu kuonekana kwake kwenye COVID klabu.

 

Sherlyne alifichua kuwa kujianika kwenye COVID kilabu, moja kwa moja kwenye Instagram iliyoandaliwa na Xtian Dela, kulimgharimu fursa nyingi kwani imekuwa ngumu kusafisha jina lake.

 

Sherlyne pia alifichua kuwa mchumba wake alighairi harusi yao baada ya familia yake kuweka jina lake kwenye google na kile alichokifanya kwenye Instagram moja kwa moja kuibuka.

 

Shakilla haogopi kupoteza mwanaume juu ya maisha yake ya nyuma au mambo anayofanya kwa sasa ili kujifurahisha.

 

Akijibu ufichuzi wa Sherlyne, Shakilla alisema kuwa atabaki mwanamke hatari na kuongeza kuwa kuna wanaume wengi ulimwenguni kwa ajili yake kuwa na wasiwasi kuhusu mmoja.

 

Shakilla alipata umaaruf wake wa kwanza katika Covid Klabu mtandaoni.

 

Aliingia kwenye uangalizi baada ya mahojiano mtandaoni na Xtiandela.

 

Katika mahojiano hayo, mtoto huyo wa wakati huo mwenye umri wa miaka kumi na tisa alidai kwamba alikuwa akijihusisha kimapenzi na baadhi ya watu mashuhuri wakubwa nchini Kenya jambo ambalo lilizua taharuki kubwa kwenye vyombo vya habari.

 

Haya hayakuchukuliwa kirahisi na vigogo wa umma waliokanusha na wengine kutishia kufungua kesi za kisheria dhidi ya Shakilla.

 

Shakilla amefichua kwenye mahojiano kuwa yeye ni sosholaiti na anatoka na wanaume kadhaa.
Mwanadada huyo mwenye msimamo mkali anapenda kujiita ‘Malkia wa mitaa’ na amekuwa akitumia ukurasa wake wa Instagram kusambaza content yake.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!