Home » Kindiki Awasili Isebania

Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki hii leo Jumatano asubuhi amefika katika kituo cha polisi cha Isebania kaunti ya Migori kwa nia ya kushughulikia masuala ya ukosefu wa usalama.

 

Waziri huyo alifika mwendo wa saa 10.30 asubuhi katika kituo cha polisi ambacho kimegonga vichwa vya habari hivi majuzi.

 

Hii ni kutokana na kuongezeka kwa mvutano huko Isebania huku wakazi wakiandamana kupinga visa vya utovu wa usalama katika mji huo.
Wenyeji hao wamekuwa wakidai kuwa hali ya ukosefu wa usalama katika eneo hilo ni mbaya.

 

Waziri Kindiki baadaye anatarajiwa kuhutubia baraza la umma katika Mji wa Isebania.

 

Maafisa wa polisi wamekuwa na wakati mgumu kudhibiti hali hiyo.

 

Watu wanne waliuawa Mei 25 na wawili walikufa siku iliyofuata katika mapigano.

 

Ingawa polisi walishutumu kundi hilo kwa kuvamia kituo hicho, wananchi walidai kuwa polisi waliwachokoza walipokuwa wakisafirisha mwili wa mfanyabiashara aliyeuawa na majambazi katika duka lake mjini Isebania.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!