Kaunti Ya Embu Tayari Kuandaa Sherehe Za Madaraka

Serikali ya Kitaifa imewahakikishia wananchi kuwa kaunti ya Embu iko tayari kuandaa sherehe za Madaraka siku ya Alhamisi.
Hafla hiyo itafanyika katika uwanja wa Moi kaunti ya Embu na itaongozwa na Rais William Ruto.
Akiwa na mkutano na wanahabari hii leo Jumatano asubuhi, kamishna wa eneo la Mashariki Paul Rotich amesema kaunti hiyo inatarajia takriban watu 10,000.
Ameongeza kuwa milango itafunguliwa mapema saa 4 asubuhi.
Amesema serikali imewekeza pakubwa katika Kaunti ya Embu ili kuhakikisha sherehe za Madaraka Day zinafaulu.
Kaunti hiyo itakuwa mwenyeji wa sherehe za 60 za Madaraka ambazo zitawashirikisha Wakenya kutoka tabaka mbalimbali katika ukumbi huo.
Kulingana naye Miundombinu imekarabatiwa tayari kuandaa sherehe hizo huku akitoa hakikisho kwa Wakenya kwamba Kaunti ya Embu iko tayari kuwakaribisha wakenya wote kesho Alhamisi