Home » Waziri Machogu Kukabiliana Na Maseneta

Waziri wa elimu Ezekiel Machogu anatarajiwa kufika mbele ya baraza la seneti hii leo Jumatano kujibu maswali kuhusu mkasa uliokumba shule ya upili ya Mukumu Girls kaunti ya Kakamega.

 

Machogu atataja hatua za kurekebisha ambazo Wizara ya Elimu imechukua ili kuruhusu kurejea kwa masomo katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Mukumu Kaunti ya Kakamega.

 

Hii ilikuwa baada ya shule hiyo kufungwa kwa wiki tatu mnamo Aprili 3, 2023, baada ya kifo cha wanafunzi watatu kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa kuendesha.

 

Aidha, Waziri huyo ataeleza jinsi wizara yake imetoa msaada kwa familia za waliofariki Zaidi ya hayo, ataeleza ikiwa wizara yake inanuia kufidia familia zilizoathiriwa na tuhuma za uchafuzi au la.

 

Mlipuko huo ulisababisha zaidi ya wanafunzi mia 124 waliolazwa katika hospitali kuu ya kaunti ya Kakamega katika kisa kinachoshukiwa kuwa kula vyakula vya sumu na maji chafu.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Afya Patrick Amoth alisema chakula kilichotumiwa na wanafunzi kilikuwa na kinyesi cha binadamu.

 

Kufuatia tukio hilo, Waziri aliteua Jane Mmbone kama mwalimu mkuu wa shule hiyo na kumhamisha Mkuu wa Shule ya Mukumu Girl Frida Ndolo.

 

Waziri huyo pia alivunja bodi ya usimamizi ya shule hiyo ambayo hadi sasa imesababisha vifo vya wanafunzi watatu na mwalimu mmoja Alifanya mabadiliko hayo alipozuru shule kutathmini hali ilivyokuwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!