Home » Noordin Haji Avuliwa Tuzo Aliyopokea 2019

Shirika la Transparency International Kenya (TIK) limeondoa tuzo ya uadilifu ya uongozi iliyotolewa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji mnamo 2019.

 

Katika taarifa yake, shirika lisilo la kiserikali la kupambana na ufisadi limebainisha kuwa kujitoa huko kulifuatia maombi ya wadau mbalimbali wanaohoji uadilifu wa Haji.

 

Katika notisi hiyo iliyotiwa saini na Sheila Masinde, Mkurugenzi Mtendaji wa TIK, imeonyesha kuwa imechunguza maombi tofauti yanayoibua wasiwasi kuhusu uondoaji wa kesi za ufisadi wa hali ya juu na kusababisha upotevu wa pesa za umma.

 

Hivyo Haji aliamriwa kurudisha cheti alilopokea sambamba na tuzo hiyo.

 

“Kwa kuzingatia maswala haya na baada ya kutafakari kwa kina, Transparency International Kenya imefanya uamuzi wa kuondoa Tuzo ya Uadilifu wa Uongozi (Afisa wa Serikali/ Umma) uliyopewa mwaka wa 2019, kwa kuzingatia imani yetu kwamba kudumisha viwango vya juu zaidi vya uadilifu ni muhimu. kwa wapokeaji wote wa tuzo zetu.

 

“Kwa hivyo tunakuhitaji urudishe cheti na bamba ulilopewa kwa ajili ya tuzo,” shirika lilisema.

 

Awali TIK ilitishia kupinga uteuzi wa Haji kama Mkurugenzi Mkuu wa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS) kumrithi Meja Jenerali Mstaafu Philip Kameru na Iliibua madai sawa na hayo yaliyomo kwenye barua ya kuondoa tuzo yake.

 

Akijibu madai yaliyoibuliwa, Haji, Jumatatu, Mei 22, aliteta kuwa ana haki na sheria kuondoa kesi ambazo hazina ushahidi wa kutosha.
Kesi hizo ambazo Haji alijiondoa zilijumuisha za ufisadi zinazohusisha Naibu Rais Rigathi Gachagua, na Mawaziri Aisha Jumwa na Mithika Linturi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!