Home » NTSA Yafuata Wauzaji Bandia Wa Mafuta Ya Magari Nchini

Picha kwa hisani

Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama (NTSA), kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu George Njau imeanzisha msako dhidi ya wafanyabiashara wote wanaowapa madereva mafuta bandia.

 

Njao amebainisha kuwa mafuta hayo pamoja na vipuri ghudhi ndiyo sababu kuu za ajali nchini.

 

Ameongeza kuwa Mamlaka imeshirikiana na wadau wakiwemo Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) ili kuhakikisha bidhaa zenye ubora pekee kwa sekta hiyo zinafika sokoni.

 

Zaidi ya hayo, amebainisha kuwa NTSA ilikuwa ikifanya kazi na kaunti 10 kuunda mipango na kamati za kukabiliana na usalama barabarani ili kusaidia kuimarisha usalama barabarani katika kaunti.

 

Njao ameeleza kuwa NTSA itashirikiana na kaunti 10 kutumia njia zisizo za magari kwa watumiaji wa barabara, kama vile kujenga barabara za abiri wanaotumia miguu.

 

Kaunti hizo pia zitakuwa na uwezo wa kuwajengea waendesha bodaboda barabara yao na uhamasishaji wa usalama barabarani.

 

Njao amesisitiza kuwa msako mkali uliowekwa na Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen unalenga kuleta utulivu barabarani na kupunguza vifo.

 

Hatua nyingine zilizoanzishwa na mamlaka hiyo ni pamoja na kuboresha alama za barabarani na kutumia plastiki zenye kaboni badala ya chuma ili kupunguza uharibifu wa alama za barabarani.

 

Njau ameandamana na mkurugenzi wa mpango wa usalama barabarani NTSA Dancun Kibogong’ ambaye alifichua kuwa vifo kwenye barabara hiyo vimepungua.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!