Aliyekuwa Kiongozi Wa Mungiki Maina Njenga Aachiliwa
Aliyekuwa kiongozi wa Mungiki Maina Njenga ameachiliwa huru na maafisa wa Idara ya upelezi na makosa ya jinai DCI kiambu.
Njenga alijiwasilisha katika makao makuu ya Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) katika Kaunti ya Kiambu hii leo asubuhi.
Walioandamana na Njenga ni akiwemo wakili wake George Wajackoya, kiongozi wa Narc- Kenya Martha Karua, Eugene Wamalwa, na aliyekuwa Gavana wa Murang’a Mwangi wa Iria.
Kulingana na Wamalwa, Njenga alisafirishwa hadi eneo lisilojulikana baada ya kuhojiwa katika makao makuu ya DCI kule Nkauru hiyo jana .
Hapo awali, polisi walitumia vitoa machozi kutawanya umati wa watu waliokuwa wamekusanyika nje ya makao makuu ya DCI.
Umati unaodaiwa kuwa wafuasi wa aliyekuwa kiongozi wa Mungiki Maina Njenga, ulitaka aachiliwe baada ya kujiwasilisha kwa DCI kuhojiwa.
Njenga alikuwa akihojiwa na polisi baada ya bunduki mbili na zaidi ya misokoto 90 za bangi kupatikana katika nyumba yake moja huko Ngomongo, Kaunti Ndogo ya Bahati.
Jana Jumatano, Njenga alifika katika Mahakama ya Nakuru na baadaye katika afisi za DCI za Kaunti ya Nakuru ambapo alirekodi taarifa Kisha alitakiwa kujiwasilisha mbele ya maafisa wa DCI jijini Nairobi leo, kwa uchunguzi zaidi.