Home » Atwoli Apuuzilia Mbali Mazungumzo Ya pande Mbili

Katibu Mkuu wa Muungano wa Muungano wa Wafanyakazi (COTU) Francis Atwoli sasa anamtaka Rais William Ruto na kiongozi wa Azimio la Umoja One wa Kenya Raila Odinga kuachana na mchakato wa mazungumzo ya pande mbili unaonuiwa kutatua tofauti kati ya upinzani na serikali.

 

Atwoli badala yake anawataka viongozi hao wawili kuondoa tofauti zao kibinafsi na kuiongoza nchi kuelekea kuimarika kwa uchumi.

 

Akizungumza wakati wa hotuba kwa wanahabari hii leo Alhamisi, mkuuhuyo wa COTU amekashifu mazungumzo yanayoendelea akisisitiza kwamba hayana umuhimu wa kuunganisha nchi.

 

Atwoli amesema wafanyikazi wa Kenya wameathiriwa zaidi na nyakati za kiuchumi zilizopo na wanakabiliwa na hatari kubwa kama vile kupunguzwa kwa nafasi za ajira, akiongeza kuwa ni viongozi wawili pekee wanaoshikilia suluhu la kukomesha hilo kutokea.

 

Matamshi hayo yalijiri baada ya Muungano wa Wazalishaji wa nafaka kutoa wito kwa Bunge kusitisha Mswada wa Fedha wa 2023, ukisema kuwa nchi inaweza kupoteza Ksh.135 bilioni na kuacha zaidi ya watu 100,000 bila kazi.

 

Atwoli hata hivyo ametetea pendekezo la Hazina ya Makazi inayopendekezwa, akisema kuwa itaondoa makazi duni na pia kuhakikisha hali bora ya maisha kwa Wakenya.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!