Home » Shule Ya Nairobi Yatoa Ekari 10 Kwa Mradi Wa Rais Ruto

Shule Ya Nairobi Yatoa Ekari 10 Kwa Mradi Wa Rais Ruto

Shule ya Nairobi imetoa ekari 10 za ardhi kuwezesha mradi wa mabadiliko ya hali ya anga wa Rais William Ruto kote nchini.

 

Akizungumza katika ziara ya kiserikali shuleni hapo, Waziri wa Elimu, Ezekiel Machogu amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kikao na viongozi wa taasisi hiyo ambao waliahidi kumuunga mkono Rais.

 

Machogu ameeleza kuwa ardhi hiyo itatumika kwa shughuli ya upandaji miti ambayo itasambaza miche kote Nairobi na maeneo mengine ya nchi.

 

Amesema kuanzia wiki ijayo, wizara itatoa miche milioni moja ya miti kwa taasisi hiyo ambayo baadaye italiepusha taifa na athari za mabadiliko ya tabianchi.

 

Aidha, Machogu amesema walimu katika taasisi hiyo wameunga mkono kwa kauli moja mpango wa makazi wa asilimia 3 na kubainisha kuwa ni faida yao.

 

Wakati uo huo, rais Ruto aliahidi kusaidia shule hiyo kwa ajili ya maendeleo ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi.

 

Kwa hali ya kuwa shule inapokea wanafunzi zaidi, rais Ruto aliahidi kuhamasisha wengine kujenga maabara ya shule hiyo, bweni na madarasa zaidi.

 

Itakumbukwa kwamba Punde tu baada ya kushika wadhifa wa urais, Ruto alianza dhamira ya kulinda mazingira, na kuahidi kusimamia upanzi wa zaidi ya miti milioni 10 katika miaka 10.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!