Home » Wizara Ya Kindiki Yajibu Kwa Kina Ripoti Ya Udukuzi Ya China

Wizara Ya Kindiki Yajibu Kwa Kina Ripoti Ya Udukuzi Ya China

Wizara ya Mambo ya Ndani imeondoa hofu yoyote kwamba mashirika muhimu ya serikali yalidukuliwa na watu kutoka Uchina wanaotafuta habari juu ya deni lao linalozidi kuongezeka.

 

Katika taarifa iliyotiwa saini na Katibu Mkuu Raymond Omollo, Wizara imeshikilia kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa miundomsingi ya kiteknolojia ya utawala wa Rais William Ruto ilidukuliwa.

 

Zaidi ya hayo, serikali imeonyesha kutoridhishwa kwake kuhusu kama China ingeweza kudukua mifumo ambayo ilinunuliwa kutoka kwa Taifa hilo la Asia ikisema kuwa haiwezekani mtu yeyote kupata data kutoka kwa serikali.

 

Wizara ya usalama imewataka Wakenya kuchukulia ripoti hizo kama propaganda.

 

Kauli hiyo imekuwa kujibu ripoti ya Reuters Media iliyodai kuwa wadukuzi kutoka China walilenga mitambo muhimu ya Serikali kuhusiana na deni kubwa.

 

Kwa upande mwingine, katibu Raymond anasema kuwa wizara inakubali kwamba udukuzi ulikuwa tishio ambalo kila serikali duniani kote ilikabiliana nayo.

 

Akijibu, Omollo amedokeza kuwa hatua mbalimbali za usalama zitaendelea kuchukuliwa ili kulinda mifumo ya kiteknolojia ya serikali.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!