Home » Haji Kupigwa Msasa Na Wabunge Wiki Ijayo

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji, ambaye wiki jana aliteuliwa kama Mkurugenzi Mkuu mpya wa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (N.I.S) Jumanne wiki ijayo atafikishwa mbele ya wabunge kupigwa msasa.

 

Katika notisi, karani wa Bunge la Kitaifa, Samuel Njoroge amesema kamati ya idara ya Bunge ya Kitaifa kuhusu Ulinzi, Ujasusi na Uhusiano wa Kigeni itaendesha zoezi hilo.

 

Timu inayoongozwa na Mbunge wa Belgut Nelson Koech itatarajiwa kuwasilisha ripoti yake kwa Bunge ili kuidhinishwa au kukataliwa mara tu vikao vitakaporejea Juni 6.

 

Wananchi sasa wana hadi Jumatatu, Mei 29, kuwasilisha maoni yao, kwa njia ya taarifa za maandishi yenye ushahidi wa kuunga mkono, kupinga au kufaa kwa mteule kuteuliwa kama mkuuwa NIS.

 

Noordin atahitajika kuwasilisha vyeti vyake rasmi kwa kamati na kitambulisho.

 

Zaidi ya hayo, atahitajika pia kupata barua kutoka kwa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC), Mamlaka ya Ushuru ya Kenya (KRA), Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELB), Kurugenzi ya Uchunguzi wa Jinai (DCI) na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

 

Haji ambaye anahudumu kama DPP wa sasa anatazamiwa kurejelea N.I.S baada ya miaka sita ya kuhudumu katika nafasi hiyo.

 

Kabla ya kuwa DPP, aliwahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha Kukabiliana na Uhalifu uliopangwa ndani ya Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi.

 

Aidha Ana Shahada ya Kwanza ya Sheria na Shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Wales, Cardiff, pia ana Shahada ya pili ya Uzamili katika Sera ya Usalama wa Kitaifa na Sifa kutoka Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Australia.

 

Haji alipata kazi katika Baraza hilo mwaka wa 1999 na baadaye akajiunga na Utumishi wa Umma Januari 2000, akifanya kazi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

 

Uteuzi wa Haji unajiri kabla ya kustaafu kwa Meja Jenerali Philip Wachira Kameru, Mkurugenzi Mkuu anayeondoka.
Kameru aliteuliwa mnamo Septemba 2014 baada ya taaluma ya kijeshi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!