Home » DJ Fatxo Afichua Maandishi Ya Mwisho Ya Jeff Mwathi

Lawrence Njuguna, almaarufu DJ Fatxo ameelezea matukio yaliyosababisha kufariki kwa Jeff Mwathi.

 

Akiongea katika kituo cha Radio Jambo , amebainisha kuwa Mwathi alionekana kufadhaika mwendo wa saa sita usiku walipokuwa wakiburudika kwenye jumba moja kando ya barabara ya Thika.

 

Wakati huo, DJ Fatxo alidokeza kuwa alikuwa amezama katika mazungumzo na mmiliki wa klabu na hakuwa akimtilia maanani Mwathi ambaye alikuwa na mpenzi wake.

 

Msanii huyo wa lugha ya Kikuyu alidokeza kuwa alipokea ujumbe mfupi kutoka kwa Mwathi ambaye aliomba Ksh.500 akisema kuwa hakua vizuri kifedha.

 

“Katika klabu, Jeff hakuwa na maelewano mazuri na mpenzi wake kwa hivyo hawakuwa wakizungumza. Baadaye nilipokea ujumbe kutoka kwa Jeff akiomba Ksh200 au Ksh500 kwa vile alikuwa hana pesa Alituma nambari ya till.

 

“Nilimtumia Ksh.500. Haikuchukua dakika chache hadi mpenzi wa Mwathi alipokuja na kunikumbatia akiniambia anaondoka. Tulishangaa kwa nini anaondoka na sherehe ilikuwa karibu kuanza,” alibainisha.

Msanii huyo alidai kuwa alimpigia simu dereva wake ili amchukue pamoja na marafiki zake katika klabu ya eneo hilo ili kuwapeleka nyumbani na kushangaa sana dereva alikuja na binamu yake.

 

Baada ya mazungumzo mafupi na Mwathi, DJ Fatxo alidai kuwa walikubaliana kwamba angekaa nyumbani kwake ili kununua vitu vinavyohitajika kwa biashara yake siku iliyofuata.

 

“Yeye (dereva) alikuja na binamu yangu na hatukuweza kuwa na watu saba kwenye gari moja hivyo nikawaambia wapande teksi na kuishia kujiendesha hadi nyumbani.”

“Dakika chache baadaye, dereva wangu na binamu yangu walifika maskaani. Mwathi aliomba pombe, ambayo nilimpa. Ilikuwa saa 4:00 asubuhi,” alikumbuka.

DJ huyo pia alisema kuwa mmoja wa wanawake waliokuwa wameandamana nao aliomba kuachwa nyumbani na akalazimika kufanya hivyo wakati akiondoka, alibaini kuwa ilikuwa mara ya mwisho kumuona Mwathi akiwa hai.

 

“Nikiwa usingizini Faith aliniamsha na kutaka kurudi nyumbani, niliamka na kuwachukua wale wanawake watatu na kuwaacha Mwathi, binamu yangu na dereva, baada ya kuwashusha nikaenda kuchukua kifungua kinywa,. saa 5:00 asubuhi, nilikuwa mlevi sana hivyo nilisinzia.Kilichoniamsha ni jua kali kwani ilikuwa saa 9:00 alfajiri.

 

“Niliporudi kwenye nyumba yangu, nilipata maafisa wa polisi na nikafahamishwa na mlinzi kwamba mtu fulani alikuwa amejitupa kutoka orofa ya 12 na sikushuku lolote kwani nilikaa kwenye ghorofa ya 10,” alisema.

 

Alibainisha kuwa aliegesha gari lake na kuendelea kuutazama mwili huo kwa muda mfupi kabla ya kuelekea kwenye nyumba yake.

“Baada ya kuegesha gari nilizuiwa na nguzo zile zisiuone vizuri mwili huo nikatazama kwa ufupi nikaona ni kichwa kimepasuka na mtu asiye na nguo fupi, kwenda nyumbani nikamkuta binamu yangu na dereva walikuwa wameamka na nikawafahamisha kuhusu mwili huo.”

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!