Home » Uhuru Aeleza Jinsi Uvamizi Wa Northlands Ulimbadilisha Mawazo

Former President Uhuru Kenyatta/Photo courtesy

Aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta amefichua ni kwa nini alikuwa bado hajastaafu kutoka kwa siasa kali miezi minane baada ya kukabidhi ala za mamlaka kwa mrithi wake, William Ruto.

 

Kenya Kwanza imekuwa ikishinikiza rais huyo wa zamani kustaafu kwa mujibu wa Sheria ya Mafao ya Kustaafu ambayo inasema kwamba aliyekuwa Wakuu wa Nchi hafai kushikilia kiti cha kisiasa ili kufaidi marupurupu yake.

 

Uhuru ambaye amekuwa akizungumza wakati wa Kongamano la Kitaifa la Wajumbe (NDC) wa Jubilee amesema kwamba hatastaafu kutoka kwa siasa.

 

Uhuru ameonya wanachama waasi wa Jubilee na wanasiasa kutoka Kenya Kwanza kwa kumshambulia kila mara.

 

Aidha, amedai kuwa alikaa kimya walipoiba mbuzi na kuchoma baadhi ya bidhaa katika shamba la familia yake la Northlands Kule Ruiru na ndicho kichocheo chake kusalia katika siasa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!