Home » Martha Karua Amuonya Rais Ruto

Kiongozi wa chama cha NARC Kenya Martha Karua amemwonya Rais William Ruto kuhusu madai yake ya kujihusisha na masuala ya muungano wa Azimio la Umoja na vyama tanzu.

 

Akizungumza wakati wa Kongamano la Kitaifa la Wajumbe (NDC) Jumatatu, Karua amemshtumu Rais Ruto kwa kutaka kutwaa chama cha Jubilee kwa nguvu na kuwa na uwakilishi wengi serikalini ili kubatilisha katiba inayompendelea.

 

Mwanasiasa huyo ameongeza kuwa shambulio dhidi ya Jubilee ni shambulio dhidi ya muungano wa Azimio na hawatakubali kuingiliwa na mtu yeyote katika kambi yao.

 

Kiongozi wa chama cha NARC amemsuta Rais Ruto kuendelea kukashfu Azimio, akionya kwamba mazungumzo ya pande mbili yatasitishwa iwapo hatua thabiti hazitakuwepo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!