Uhuru Awatimua Wanachama 10 Jubilee
Aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta amekabiliana vikali na wanachama walioasi alidai hawakuwa waaminifu kwa chama.
Akizungumza katika Uwanja wa Ngong Racecourse wakati wa Kongamano la Kitaifa la Wajumbe wa chama (NDC), Uhuru amebainisha kuwa wanachama hao walikiuka katiba ya chama kwa kuendeleza ajenda za vyama vingine vya kisiasa nje ya muungano wa Azimio la Umoja.
Kupitia kwa Katibu Mkuu wa Jubilee Jeremiah Kioni, kiongozi huyo amewatimua wanachama wafuatao kutoka nyadhifa zao mbalimbali:
Jimmy Angweny, Mbunge wa zamani wa Buuri Boniface Kinoti Gatobu, Naomi Shaban, Nelson Dzuya, Joshua Kutuny, Mutava Musyimi na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Kanini Kega.
Rachael Nyamaye, Advice Mundalo, Mkurugenzi Mtendaji Wambui Gichuru na Joel Kibe pia hawakusalia.
Aidha wanachama kumi wamechukua nafasi za wale waliotimuliwa.
Majina yaliyopendekezwa ya Chama cha Jubilee ni pamoja na;
Naibu kiongozi wa mkakati: Beatrice Gambo
Operesheni za naibu kiongozi wa chama: Maoka Maore
Naibu kiongozi wa chama wa mipango Joseph Manje
Naibu kiongozi wa chama – Kados Muiruri
Mwenyekiti- Saitoti Torome (PS)
Naibu katibu mkuu – Yasir Noor
Naibu Katibu Mwenezi – Pauline Njoroge
Mkurugenzi wa Kitaifa wa Uchaguzi – Jamleck Kamau
Mwenyekiti wa Wanawake Taifa – Maison Leshomo
mwenyekiti wa Taifa vijana, – Agnes Thumbi
Mratibu wa huduma za Vijana – Anthony Manyara
Baraza la Biashara – Nderitu Mureithi
Katibu wa Bunge – Amina Siyad