Home » ODPP Yazindua Mfumo Wa Kidigitali Kwa Wakenya

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) hii leo Jumatatu imezindua mfumo wa kidijitali kwa Wakenya kuwasilisha malalamishi na kuomba uhakiki wa kesi mtandaoni.

 

Jukwaa hilo linaloitwa (Mfumo wa Malalamishi), linawaruhusu wananchi kuwasilisha malalamiko ya asili ya uhalifu kwa ODPP na pia kuripoti bila majina yao rasmi kupitia mfumo huo.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo katika Mahakama ya Nairobi, Eneo la Viwandani,, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji amesema hii itatoa nafasi kwa watoa taarifa na kurahisisha kufuatilia hali ya malalamishi kwa vile nambari ya marejeleo imetolewa.

 

Kwa ujumla, Mfumo wa Malalamishi umewekwa kusaidia ODPP katika kutoa huduma kwa urahisi kwa wanajamii mchana na usiku, pamoja na kutafuta kwa haraka malalamishi ya wakenya kuhusiana na kesi zitakazopigwa msasa.

 

Wakati huo huo, ODPP imezindua mpango wa ‘All for Justice”, ambao unalenga kupunguza msongamano wa magereza na kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani kote nchini.

 

All for Justice Awamu ya Kwanza ilianza mwaka 2018 ili kuhoji sababu za kucheleweshwa wa kesi za jinai, hali iliyosababisha msongamano magerezani.

 

Haji vile vile amesema awamu ya pili pia itahakikisha uendeshaji wa mashtaka unazingatia zaidi mahitaji ya mwananchi, hivyo kutoa nafasi ya pili kwa walio rumande kujirekebisha na kurejeshwa kwenye jamii.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!