Home » Mzozo Wa Ardhi Wazuka Shakahola

Viongozi wa jamii kutoka Kaunti Ndogo ya Magarini katika Kaunti ya Kilifi wamedai umiliki wa ardhi inayodaiwa kumilikiwa na mchungaji Paul Mackenzie la ekari 840 la Shakahola.

 

Viongozi hao wakiongozwa na wazee wa Mjikenda Kaya wamesema sehemu ya ardhi ambayo ina misitu mkubwa ni msitu wa jamii ya wazee wa Magarini Kaya.

 

Aidha Wamelaani ibada ya mfungo ya Paul Mackenzie kwa kusababisha mamia ya vifo vikiwemo vya watoto na wanawake na sasa wanataka serikali iwaachilie ardhi hiyo ili wasafishe mara tu uchunguzi unaoendelea utakapokamilika.

 

 

Tsuma Nzai kutoka Magarini amesema kuwa mchakato wa utakaso huo utahusisha utafiti wa jina la Shakahola na maana yake ili liweze kubadilishwa,kulaani eneo hilo kisha kulisafisha kwa mujibu wa haki za utakaso za Mijikenda.

 

Said Matojo kutoka jamii ya Bobo huko Rabai amesema kuwa kuachwa kwa shughuli za kidini asilia za Kiafrika na kukumbatia shughuli za kidini za kigeni ndio chanzo cha matatizo yote yanayoyatia doa mataifa.

 

Wakati uo huo, Wabunge wa Malindi na Magarini, Amina Mnyazi na Harry Kombe wameitaka serikali kuwianisha maeneo ya utawala ili kuendana na maeneo bunge wakisema kuwa eneo la uhalifu la Shakahola liko katika Kaunti Ndogo ya Malindi lakini katika Kaunti Ndogo ya Magarini.

 

Kombe amependekeza kuwa mipaka hiyo inafaa kuangaliwa upya ili Kaunti Ndogo ya Malindi iwe eneo bunge la Malindi na Kaunti Ndogo ya Magarini iwe eneo bunge la Magarini.

 

Mnyazi kwa upande wake amesema inasikitisha kwamba watu walikuwa wanahusisha Shakahola na yeye huku bado eneo hilo liko katika jimbo la Magarini.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!