Home » Mchungaji Ezekiel Apata Afueni

Ni afueni kwa kasisi Ezekiel Odero baada ya akaunti zake za benki ambazo zilifungiwa Mei 8, 2023, kufunguliwa.

 

Leo hii Jumatatu, mahakama imeambiwa kuwa benki tano Cooperative, NCBA, Equity, KCB na HFC kufungua akaunti hizo rasmi ambapo zimetii agizo hilo na kuruhusu uchunguzi wa akaunti mbalimbali za mhubiri huyo.

 

Akiwa anahojiwa na Wakili Danstan Omari, Inspekta Martin Munene ameambia mahakama kwamba kutokana na hati zilizopokelewa hakuna akaunti yoyote ya benki iliyo na jina la mchungaji Ezekiel Badala yake, akaunti zote zilikuwa za kanisa au shule.

 

Mchungaji Ezekiel sasa yuko huru kupata akaunti zake baada ya muda wa siku 15 uliotolewa na mahakama kutokamilika.

 

Hapo awali, maafisa wa upelelezi na makosa ya jina DCI walikuwa imeomba mahakama kuongeza muda wa maagizo ya kufungia akaunti ili kuruhusu Safaricom kutii maagizo hayo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!