Madaktari Wa Mifugo Washtumu Malipo Duni

Madaktari wa mifugo nchini Kenya wameelezea wasiwasi wao juu ya kiwango cha chini cha malipo yao, wakiomba serikali ya Kitaifa kuingilia kati.
Madaktari hao kupitia shirika la (Kenya Veterinary Association, ) wametoa wito kwa serikali kutoa motisha na malipo mazuri kama njia ya kuongeza ari ya maafisa wa mifugo nchini.
Chama hicho ambacho huleta pamoja uanachama wa kitaaluma kwa madaktari wote wa mifugo nchini Kenya katika sekta za umma na za kibinafsi zilizosajiliwa chini ya Sheria ya Vyama Sura ya 108 ya Sheria za Kenya kina madaktari elfu 3,000 wa upasuaji wa mifugo wanaotambulika katika kaunti 47.
Kulingana na chama hicho, uhaba wa pesa katika kaunti mbalimbali umetishia kulemaza huduma za mifugo kwani madaktari wengi wamekaa miezi kadhaa bila mishahara.
Wakiongozwa na mwenyekiti wake Nicholas Muyale, madkatri hao sasa wanataka serikali ya kitaifa kutoa pesa za kaunti kwa wakati.
Katika kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha mbwa, madaktari wa mifugo wamesema kuwa kuna haja ya mbinu za upasuaji kutumika ili kuhakikisha kuwa paka na mbwa kukoma kuongezeka zaidi ya kiwango cha usimamizi wa wamiliki wao.
Demesi Mande, mkuu wa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Nairobi na mjumbe wa bodi Mifugo ya Kenya (K.V.B), amesema kuwa kuna njia kadhaa salama za kuondoa viungo vya uzazi vya paka na mbwa katika kudhibiti uzazi wao.
Kulingana na Naibu Mkurugenzi katika Kurugenzi ya Huduma za Mifugo, Dkt Charles Ochodo, mbwa wanazaliana sana na walikuwa na uwezo wa kuzaa watoto watano hadi kumi wakati wowote na hivyo kuwalemea wamiliki wao.
Ameongeza kuwa siku za nyuma wamiliki wa mbwa hao waliishia kutumia vitendo visivyo vya kibinadamu mfano sumu, silaha ili kuwaondoa.
Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa K.V.B Dk Mary Agutu amekiri kupitishwa kwa kozi za mifugo na wasichana akisema kuwa ni jambo sahihi kuweka usawa wa kijinsia katika taaluma hiyo.