Home » Murkomen Ashtumu Wakenya

Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen ameshutumu Wakenya wanaoweka shinikizo kwa madereva wa matatu wanapokuwa barabarani.

Akizungumza, Waziri huyo amesema kuwa ‘utamaduni wa haraka’ ndio unaosukuma madereva wengi kuwa na mwendo wa kasi katika barabara kuu na na kusababisha ajali nyingi.

 

Ameeleza kuwa kuna matukio fulani ambapo baadhi ya Wakenya wanapendelea kupanda magari ambayo kimuonekano wanaweza kuona yana hitilafu badala ya kusubiri gari linalofuata linalofaa kuwa barabarani.

 

Takriban watu elfu 21,760 walihusika katika ajali za barabarani mwaka jana, kulingana na Mamlaka ya Kitaifa ya Usafiri na Usalama.

 

Aidha nayo mamlaka ya usalama barabarani NTSA ilisema watu elfu 4,690 walikufa huku wengine wakisalia zaidi na majeraha makubwa watakayoishi nayo maishani mwao.

 

Ili kuzuia ajali za barabarani, Murkomen mnamo Machi alipiga marufuku kusafiri usiku kwa mabasi ya shule.

 

Aliongeza kuwa washikadau wote wakiwemo wahudumu wa usafiri wa umma, wale wa vidhibiti mwendo, na Huduma ya Kitaifa ya Polisi NPS watajumuishwa katika zoezi hilo na mashirika mengi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!