Home » Chama Cha Jubilee Chataka Kurejeshwa Kwa Adan Keynan

Huku mazungumzo ya pande mbili yakianza leo huko katika ukumbi wa Bomas, chama cha Jubilee kimeiandikia barua kamati teule ya pamoja kupitia ‘Katibu Mkuu’ wake, Kanini Kega, kupinga kutengwa kwa uwakilishi wa chama cha Jubilee katika mapendekezo ya uanachama wa kamati teule ya pande mbili.

 

Chama hicho kimetaka kutojadiliwa zaidi kuhusu mapendekezo ya mazungumzo ya pande mbili hadi pale matakwa ya chama chao yatakaposhughulikiwa.

 

Hata hivyo, kamati ya pande mbili ambayo barua hiyo iliandikiwa ilianza kujadiliwa leo bila kuzingatia matakwa ya chama cha Jubilee.

 

Kenya Kwanza ilitangaza mapema mwezi Mei kwamba imemteua mbunge wa Saku Dido Rasso kuchukua nafasi ya mbunge aliyondolewa wa Eldas Adan Keynan katika kamati ya mazungumzo ya pande mbili.

 

Haya yanajiri baada ya muungano wa Azimio, katika barua yake ya awali, kutangaza kuwa iko tayari kusitisha maandamano yake ya kupinga serikali kesho Alhamisi kama Kenya Kwanza itakubali matakwa yake kwa Keynan kuondolewa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!