Home » Vitambulisho Sasa Kupatikana Ndani Ya Siku 21

Vitambulisho Sasa Kupatikana Ndani Ya Siku 21

Wakenya sasa wanaojisajili kupata vitambulisho vipya watapokea ndani ya siku 21 kulingana na hatua iliyopigwa na serikali.

 

Katibu Mkuu wa Uhamiaji na Huduma kwa Raia Julius Bitok leo Jumatano amesema ratiba hiyo inanuiwa kuharakisha utoaji wa vitambulisho huko Mandera na kaunti zingine za mpakani.

 

Alikuwa akizungumza huko Lafey, Kaunti ya Mandera, wakati wa ufunguzi wa afisi ya Huduma za Usajili wa Kiraia (C.R.S) kwa ajili ya utoaji wa vyeti vya kuzaliwa.

 

Wiki iliyopita, katibu huyo alitangaza kuwa vyeti vya kuzaliwa na vyeti vya vifo sasa vitashughulikiwa siku iyo hiyo ya maombi.

 

Katika asilimia 13 na 6 ya usajili wa kuzaliwa na vifo mtawalia, Mandera ni miongoni mwa viwango vya chini zaidi nchini kutoa huduma hizo huku Wastani wa kitaifa ukiwa ni kati ya asilimia 86 na 55 mtawalia.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!