Home » Hamisa Mobetto Azama Penzini

 

Mfanyabiashara na mwanamitindo Hamisa Mobetto ameingia katika penzi jipya na Ali Kamwe ambaye pia ni msemaji wa klabu ya soka ya Young Africans Sport Club baada ya ukimya wa muda mrefu wa kutokuwa katika mahusiano.

 

SOMA PIA:Hamisa Mobetto Adai Analea Wanake Pekee Yake

 

Taarifa hiyo imejiri baada ya siku chache zilizopita wawili hao wakichapisha picha mblimbali katika kurasa zao za Insta Stories huku machapisho hayo yakiwa na jembe mbalimbali za mapenzi juu ya penzi hilo.

 

 

Hali kadhalika, wapo watu waliongeza shauku ya mashabiki kutaka kufahamu zaidi juu ya wawili hao. Naye si mwingine bali ni Meneja wa masuala ya kidigitali wa klabu ya Yanga

 

Priva amekuwa akiweka utani pamoja na kutoa maoni katika kurasa hizo za Instagram na amekuwa akimuita Hamisa Shemeji.

 

Mbali na kuwa mwanamitindo lakini pia Hamisa ni mwanamuziki ambaye ana watoto wawili aliobarikiwa huku mtoto wa kwanza wa Hamisa alifanikiwa kumpata na Mkurugenzi wa EFM Majizzo na mtoto wa pili alifanikiwa kumpata na mwanamuziki Diamond Platnumz.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!