Wafuasi Wa Mchungaji Ezekiel Wakusanyika Nje Ya Mahakama Ya Shanzu
Kumeshuhudiwa kizaazaa nje ya Mahakama ya Shanzu Mombasa leo hii Jumanne, Mei 2, baada ya mamia ya wafuasi wa Mchungaji Ezekiel Odero kukusanyika katika mahakama hiyo.
Wakiongozwa na msaidizi wake ambaye pia ni kakake Mchungaji Gillack Odero, walipinga kukamatwa kwake kwa kuomba aachiliwe.
Kasisi Ezekiel Odero na kasisi Paul Mackenzie wanatarajiwa kufika mbele ya mahakama ya Shanzu leo hii kwa mashtaka ya itikadi kali, ugaidi, mauaji ya halaiki na utakatishaji fedha.
Gillack alionekana akiamuru umati mkubwa wa watu wakati akiwaongoza katika kuimba, huku mara kwa mara wakiwasihi maafisa wa polisi kuachilia Ezekiel.
Mnamo Jumapili, Gillack aliwahakikishia wafuasi wa Ezekiel kuwa watulivu akionyesha imani kwamba kanisa la kasisi huyo lililokumbwa na utata eneo la Mavueni, Kaunti ya Kilifi, litafunguliwa tena hivi karibuni.
Ezekiel alikamatwa Alhamisi, Aprili 27, baada ya Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuanza kufuatilia uhusiano wake na Mauaji ya Shakahola.
Mara tu baada ya kukamatwa, Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki alitangaza kwamba mwinjilisti huyo maarufu atashtakiwa kwa mauaji ya halaiki ya watu