Home » Rayvanny Amshusha Diamond Platnumz YouTube

Kutoka nchini Tanzania, msanii na bosi wa lebo wa Next Level Music, Rayvanny hivi karibuni ameweka rekodi mpya baada ya kuwa msanii aliyetazamwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube kwa mwezi wa Aprili na kumshusha Diamond Platnumz.

 

SOMA PIA:Rayvanny Tattoos Fahyma On His Hand

 

Kwa muda mrefu sasa Diamond Platnumz ndiye msanii kinara kwenye mtandao wa Youtube ambapo kwa mwaka 2023, Rais huyo wa WCB amekuwa ndiye msanii aliyetazamwa zaidi Youtube kwa mwezi Januari,Februari na Machi lakini kwa mwezi April mambo yameonekana kubadilika.

 

Rayvanny amshusha Diamond Youtube

Kwa mwezi April, Rayvanny amekusanya views takriban Milioni 40 Youtube hivyo kuwa msanii kutoka Tanzania ambaye ametazamwa zaidi Youtube akifuatiwa na Diamond Platnumz ambaye amekusanya views Milioni 35 kwa mwezi huo wa Aprili.

 

Rayvanny alitumia ukurasa wake wa Instagram kuzungumzia ushindi wake huo mpya ambapo amewashukurj mashabiki kwa mchango wao katika muziki wake na pia kumtania Diamond Platnumz kutokana na ushindi wake huo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!