Home » Diamond Atengeneza Historia Kwenye Video Ya Zuchu “Utaniua”

Zuchu x Diamond Utaniua

Mwanamuziki kutoka nchini Tanzania Diamond Platnumz amejiongezea cheo kingine kwenye muziki wake baada ya hivi karibuni kuwa muongozaji yaani Director wa video mpya ya Zuchu ya kuitwa Utaniua.

 

SOMA PIA:Zuchu Awafunika Tiwa Savage Na Ayra Starr

 

Video ya Utaniua ya kwake Zuchu imetoka saa chache zilizopita ikiwa ni video yake ya pili kwa mwaka huu baada ya kuachia Napambana mapema mwaka huu.

 

Video ya Utaniua imepambwa na stori nzuri ambayo inamuonesha Zuchu akiwa ni binti kutokea familia ya kihindi anayeamua kutoroka na kijana ampendaye ambaye ni Diamond Platnumz siku ya harusi yake.

 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Zuchu alidokeza kuwa video hiyo ya Utaniua imeongozwa na Diamond Platnumz huku Director Joowzey akiwa amehusika katika kuchukua picha za video hiyo ambayo kufikia sasa imeshatazamwa takriban mara laki 8 kwenye mtandao wa Youtube.

 

Utaniua ni video ya nne ambayo Diamond Platnumz na Zuchu wameshiriki kwa pamoja. Video nyingine ni pamoja Litawachoma, Cheche pamoja na Mtasubiri ambayo ilifungiwa na Baraza La Sanaa Tanzania yaani BASATA mapema mwaka jana.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!