Home » Maandamano Kurejea Jumanne Ijayo

Muungano wa Azimio la Umoja One-Kenya umeshikilia kuwa maandamano kubwa kote nchini yataanza tena Jumanne wiki ijayo.

 

Muungano unaoongozwa na Raila Odinga umeshtumu utawala wa Kenya Kwanza kwa kutojitolea kwa mazungumzo ya pande mbili na kuongeza kuwa maandamano yataendelea hata mazungumzo yakiendelea.

 

Raila Odinga jana Ijumaa alitangaza kurejelea maandamano ya mitaani ili kuishinikiza serikali kushughulikia gharama ya juu ya maisha kupitia kurejeshwa kwa programu za ruzuku ya unga, mafuta, umeme na karo za shule miongoni mwa mambo mengine.

 

Akizungumza Kibra, baada ya kurejea kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu, Odinga alisema upinzani unasimama na tangazo lake kwamba maandamano dhidi ya serikali yataanza tena baada ya Ramadhani.

 

Kiongozi wa Azimio pia alishikilia kuwa Mwanachama wa Pokot Kusini David Pkosing atasalia katika jopo la kamati ya pande mbili za Azimio.

 

Wakati huo huo Odinga alitaka uchunguzi wa kina ufanywe kuhusu mauaji ya shakahola.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!