Home » Hofu Yatanda Maambukizi Ya Ukimwi Yakiongezeka Nakuru

Kaunti ya Nakuru imerekodi ongezeko la idadi ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi miongoni mwa vijana, hii ni kwa mujibu wa takwimu za hivi punde za serikali.

 

Kulingana na ripoti iliyotolewa na Baraza la Kitaifa la Kudhibiti Magonjwa ya Sindemic (N.S.D.C.C), vijana mia 297 wenye umri wa kati ya miaka 10-19 waliambukizwa virusi vya ukimwi, na hivyo kuchangia takriban asilimia 20 ya visa vipya vilivyorekodiwa katika kaunti mnamo 2021, ambavyo vilifikia elfu 1,496.

 

 

Ripoti hiyo imeonyesha kuwa kaunti ndogo nne zilichangia asilimia 52 ya maambukizo ya virusi vya ukimwi ambazo ni; Naivasha iliripoti visa 59, Nakuru Magharibi (36), Nakuru Kaskazini (300 na Njoro (29).

 

Mkurugenzi Mtendaji wa N.S.D.C.C, Dk Ruth Masha ametoa wito kwa viongozi kusaidia kutokomeza mila na desturi zinazowaweka vijana kwenye mimba za utotoni, na ukatili wa kijinsia.

 

Akizungumza katika hafla ya uhamasishaji katika Shule ya Msingi ya Davison katika kaunti ndogo ya Njoro, Dkt Masha aliorodhesha umaskini, unyanyasaji wa mapema wa ngono, utumizi wa dawa za kulevya na ngono ya kibiashara kuwa baadhi ya mambo yanayozidisha mzigo wa vitisho mara tatu.

 

Ripoti hiyo imesema kuwa asilimia 54.3 ya wanawake walijua jinsi ya kuzuia maambukizi ikilinganishwa na asilimia 35.1 ya wanaume. Baadhi ya hatua za kuzuia ni pamoja na matumizi ya kondomu na upimaji wa kawaida.

 

Licha ya kupungua kidogo kwa visa vya ujauzito miongoni mwa vijana walio na umri wa kati ya miaka 10-19, suala hilo bado linasumbua sana, haswa kwa wale walio na umri wa kati ya miaka 10 na 14 itakumbukwa kwamba Kaunti iliripoti visa elfu 8,426 mwaka jana kutoka elfu 11,469 viilivyorekodiwa mnamo 2021.

 

Wakati uo huo, matukio ya unyanyasaji wa kingono na kijinsia (S.G.B.V) yameongezeka, huku asilimia 42 ya visa elfu 2,529 vilivyosajiliwa katika kaunti mwaka jana vikihusishwa na vijana katika kundi la umri wa miaka 10-17.

 

Kaunti ndogo ya Nakuru Mashariki iliongoza orodha ya visa vingi vya S.G.B.V vilivyorekodiwa na mia 232, huku Naivasha, Njoro na Nakuru Magharibi zikifuatia kwa visa mia 211, mia 204 na mia 160, mtawalia.

 

Gavana susa Kihika alitoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano thabiti na kutanguliwa kwa juhudi za kitaifa na kaunti katika kukabiliana na janga hilo .

 

Viongozi wa serikali ya kitaifa na kaunti akiwemo Mkuu wa Mkoa na wafanyakazi wa kujitolea wa afya ya jamii walihimizwa kuendeleza mijadala yenye kujenga kuhusu suala hilo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!