Home » Meja Kunta Aachia Ngoma Mpya “Ushali”

Ushali, Meja Kunta

 

Msanii nguli wa Singeli kutokea Tanzania, Meja Kunta ameachia ngoma yake mpya kabisa ya kuitwa Ushali. Huu ni wimbo wa nne wa Meja kuuachia tangu kuanza kwa mwaka huu.

 

SOMA PIA:Meja Kunta Awashirikisha Marioo, Mabantu katika Demu Wangu Remix

 

Kwenye ngoma hiyo, Meja Kunta ameshirikisha mafundi wawili wa Singeli ambao ni Kidochu Mc pamoja na Elisha ambao wameongeeza vionjo na  wamenogesha zaidi wimbo huo.

 

 

Kimashahiri, Ushali ni ngoma ambayo ni kama muendelezo wa ngoma yake ya “Demu Wangu” kwani ndani ya ngoma hii, Meja Kunta anatoa vitisho na maneno ya kuudhi kwa mpenzi wake ambaye amemtaarifu kuwa anataka waachane.

 

Kama ambavyo “Demu Wangu” ilifanya vizuri, Ushali pia inatarajiwa kufanya vizuri kwenye mitandao ya kusikiliza na kupakua muziki.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!