Home » Meneja Afichua Jinsi Country Wizzy Alivyokutana Na Emtee Wa Afrika Kusini

Kama kuna wimbo wa Hip hop ambao unafanya vizuri sana kwa sasa basi ni “Oright” wa kwake rapa Country Wizzy akiwa amemshirikisha nguli wa Hip hop kutoka huko kwa Madiba Emtee.

 

SOMA PIA:Diamond Platnumz Na Shilole Wateuliwa Na Rais Samia

Ngoma ya “Oright” ya kwake Country Wizzy imekuja kama “surprise” kwa mashabiki wengi hasa ukizingatia kuwa Country amemshirikisha msanii wa kimataifa, Emtee.

 

 

Emtee ni rapa anayehishimika sana huko Afrika Kusini ambaye ameshafanya kazi na wasanii kama Tiwa Savage, Nasty C, Wizkid, AKA na wengineo wengi huku akiwa ameshinda tuzo kubwa za kimataifa kama South African Hip Hop Awards na Global Music Awards Africa.

 

Akizugumza hivi karibuni, meneja wa Country Wizzy amedokeza kuwa rapa huyo alienda Afrika Kusini kwa ajili ya kupata collabo na Nasty C lakini kutokana na kupishana kwa ratiba, Nasty C hakuwepi na ndipo hapo wakapata nafasi ya kukutana na Emtee studio kupitia Mulla ambaye ni rafiki wa Country Wizzy.

 

“Lengo lilikuwa ni kushoot some videos na na kupata collaboration na Nasty C lakini kipindi kile Nasty C alikuwa nje ya nchi na kwa muda mrefu Country alikuwa na ndoto ya kufanya kazi na Emtee hivyo tulikutana na Emtee kupitia Mulla.”

 

Meneja huyo alidokeza pia kwamba video ya ngoma hiyo ipo tayari na inatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!